18 Januari 2026 - 23:06
Source: IQNA
Rais Pezeshkian asema Marekani na Israel zimehusika moja kwa moja katika machafuko Iran

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuhusika moja kwa moja Marekani, utawala wa Kizayuni na baadhi ya nchi za Ulaya katika matukio ya hivi karibuni ya Iran hakukanushiki.

Rais Masoud Pezeshkian amesema hayo kwenye mazungumzo ya simu na Rais Vladimir Putin wa Russia na huku akipongeza msimamo wa Moscow wa kuiunga mkono Iran katika Umoja wa Mataifa na majukwaa mengine ya kimataifa, amezungumza kwa muhtasari kuhusu matukio ya siku chache zilizopita humu nchini na jinsi Marekani, utawala wa Kizayuni na baadhi ya nchi za Ulaya zilivyoshiriki moja kwa moja kwenye matukio hayo.

Amesema, mbinu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika sera za ndani ni kuimarisha wananchi wake na kuwashirikisha kikamilifu katika kutatua masuala yao. Kwa upande wake, taifa kubwa la Iran, lililo imara na lililo macho, limefanikiwa kuwasambaratisha wachocheaji na wafanyaji ghasia kwenye maandamano hayo.

Habari inayohusiana:

Ayatullah Khamenei: Iran haitalegeza msimamo na itakabiliana na magenge ya wahalifu
Kwa upande wake, Rais Vladimir Putin wa Russia ameelezea kufurahishwa kwake na kupata fursa ya kuzungumza na Rais Pezeshkian na ametuma salamu zake za dhati wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei. Amesema kwamba Russia inafuatilia matukio ya nchini Iran kwa uangalifu na kwa umakini na kusema kuwa, yaliyojiri nchini Iran katika siku za hivi karibuni ni sawa na matukio ya mapinduzi ya rangi yaliyotokea katika baadhi ya nchi. Amesema: Tunaelewa kikamilifu kwamba matatizo ya kiuchumi na kijamii yatatokea nchini Iran kutokana na athari za vikwazo vya muda mrefu vya madola ya Magharibi, lakini machafuko na vurugu hazina uhusiano wowote na maandamano ya amani na ya kiraia.

Your Comment

You are replying to: .
captcha